Mwandishi wetu
EDIMUND Josephat (30) mkazi wa kata ya Kaloleni mkoani Songwe ametajwa
kupoteza maisha kutokana na unywaji wa pombe kali.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Mathias Nyange amesema kijana huyo
alikutwa nyumbani kwake eneo la Mgombani Desemba nne mwaka huu saa tatu usiku
akiwa amefariki dunia.
Kamanda huyo amesema
ilithibitika kuwa kijana huyo alipoteza maisha kutokana na Unywaji pombe kali
baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari na kubaini kuwa pia
alikuwa hajala chakula.
Hata hivyo Kamanda Nyange amesema bado haijabainika ni aina gani
ya Pombe kali aliyokunywa hata ikapelekea umauti kijana huyo huku pia jeshi la
polisi likiendelea na uchunguzi juu ya kifo hicho ikiwamo kufuatilia ni wapi
alikokuwa akinywa pombe.
0 Michango:
Post a Comment