Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Democrasia na Maendeleo (Chadema) |
Mwandishi wetu
CHAMA cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), kimesema kitabudi njia nyingine zingine za kufanya
siasa na kukutana na wananchi licha ya Rais John Magufuli kupiga marufuku
mikutano ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020.
Tundu Lissu, Mwanasheria
Mkuu wa Chama hicho ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya
siasa kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambao wako nchini kwa ziara ya mafunzo
ya kisiasa.
“Sisi ni wanasiasa na hiyo ndio kazi yetu,
sasa kama Rais amepiga marufuku tufanyeje? Hatuwezi kwenda kanisani eti
tukasali ili turuhusiwe kufanya mikutano ya hadhara, tunachofanya ni kubuni
mbinu zingine za kukabiliana na watawala na si kujifungia ndani na kukaa
kimya,” amesema Lissu.
Amesema kuwa njia
ambazo Chadema imepanga kufanya ili kuhakikisha chama kinaendelea kufikia
wanachama wake na wananchi, ni vikao endelevu vya ndani ambapo walianza juma
lililopita kwa kanda za Kati na Kusini.
Hata hivyo amesema Chama
chochote cha siasa kinapaswa kujifunza kuishi katika mazingira ya kila aina,
hivyo ili kuhakikisha Chadema inaendelea kuwa hai ni lazima ibuni njia
mbalimbali za kufanya siasa.
0 Michango:
Post a Comment