//
Ads

Anna Mghwira asisitiza kuitekeleza Ilani ya CCM



"MPAKA sasa mimi ni mwenyekiti wa chama, nitakaa na wenzangu tuangalie mazingira ya chama chetu jinsi kilivyo kutokana na majukumu yangu nitakuwa Kilimanjaro kwa muda mwingi uwenyekiti wangu itakuaje"

Ni kauli ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Anna Mgwira alipokuwa kwenye mahojiano na Azam Tv jana mara baada ya kuapishwa kwenye nafasi ya ukuu wa Mkoa huo, ambapo amesisitiza kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo.

Amesema kuwa uenyekiti wa chama chochote nchini ni sharti uwe na Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar na makamu wake wote wanaimudu nafasi ya umakamu.

" Ilani ya chama cha mapinduzi ni lazima niitekeleze, napotekeleza Ilani nikiona ina mapungufu namuona Mwenyekiti wa chama na Katibu wake kwamba Ilani hii haitekelezeki.


"Wakati mwingine hizi Ilani watu wanaongea tu maneno hawazisomi, Ukiisoma Ilani ya kila chama cha Tanzania zote ni nzuri,"
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment