//
Ads

Rc Mongella-Wenyeviti, Madiwani ni wapiga dili

Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella.
Na Mwandishi wetu
JOHN Mongella, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, amesema kuwa wenyeviti wa Halmashauri na baadhi ya madiwani mkoani humo wameshindwa  kutekeleza majukumu yao ya kusimamia miradi ya maendeleo na badala yake wamegeuka wapiga dili.
Mongella amesema wenyeviti hao na madiwani wamekuwa wakishindwa kusimamimia miradi ya maendeleo na badala yake wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wakuu wa idara ili wasiwachukuliwe hatua pindi wanapobainika tuhuma.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua mkutano wa robo mwaka wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (Alat) mkoani hapa, ambapo alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha miradi mingi ya maendeleo kukwama.
Amesema kuwa baadhi ya madiwani wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa watendaji hususan wakuu wa idara ili pale wanapobainika miradi ya maendeleo waliosimamia imejengwa chini ya kiwango, waweze kuwatetea na kuwaonya kuacha mchezo huo.
Mongella ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama mkoa, amesema kuwa hali hiyo pia imekuwa ikichangia baadhi ya wakuu wa idara kwa kushirikiana na madiwani kuandika taarifa za uongo za halmashauri yao pindi zinapohitaji serikali kuu.
"Mfano hapa Ukerewe kuna taarifa nyingi za uongo zinazoandikwa na hiyo yote inatokana na madiwani kushindwa kutambua wao wapo kwa ajili ya wananchi lakini kila siku ukienda halmashauri unawakuta na wanachukua Sh. 20, 000 kutoka kwa watendaji.
"Kama unachukua hizo hela alafu kesho unadhani utamchukulia hatua zozote na miradi iliojengwa chini ya kiwango haitakosekana kwa sababu tayari diwani umechukua pesa tayari ni lazima kuacha vitendo hivyo.
"Miradi ya wadhabuni na ya halmashauri kuu inakwama kwa sababu ya upigaji dili, kuna nyumba hapa (Ukerewe) kwenye taarifa imeandikwa imekamilika lakini haijakamilika na hata kwenye ripoti ya CAG (Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali) na yeye kaandika imekamilika kwa sababu alidanganywa," amesema Mongella.
Hata hivyo, amesema baadhi ya madiwani na wenyeviti wa Halmashauri mkoani hapa pindi wanapopata nafasi wamekuwa wakishindwa kufanya kazi walizoomba na badala yake huendekeza rushwa kwa lengo la kupata pesa kwa muda mchache.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment