![]() |
Waandishi wa habari |
Na Mwandishi wetu
IMETABIRIWA kuwa mwaka
huu 2017 huenda ukawa mbaya kwa upande wa waandishi wa habari kutokana kukumbwa
na vifo kama ilivyo tokea mwaka jana ambapo paa la tasniua hiyo
duniani kote alitua bundi.
kwenye utabiri huo
wametajwa viongozi wakubwa wa upinzani duniani ikiwamo Tanzania wametabiriwa
kurejea kwenye vyama walivyovihama mwaka huu.
Utabiri huo ulitolewa
jana na mtabiri Maalimu Hassani Yahya Hussein ambaye ni mtoto wa Sheikh Yahya
Hussein aliyekuwa mnajimu wa kimataifa ambapo ametoa utabiri huo wa mambo 20
yatakayotokea mwaka huu.
Mtabiri huyo pia
alikitabiria kifo chama kimoja cha upinzani maarufu hapa nchini na anguko la
vyama tawala katika nchi mbalimbali duniani.
“Chama Cha Mapinduzi
kitashika hatamu zaidi itakayoleta maendeleo makubwa pia kuimarika kwa hali ya
uchumi duniani kote ikiwamo Tanzania na hali ngumu iliyokuwapo mwaka jana
kutoweka.
“Natabiri Rais Dk.
John Magufuli kupata nishani ya juu ya dunia kutoka kwa Rais wa moja ya mataifa
makubwa duniani kutokana na uongozi wake,” alisema Maalimu Hassan.
Alisema kutatokea
mvutano wa kimtazamo na sera utakaosababisha mabadiliko makubwa ya uongozi wa
kiserikali duniani na Tanzania ikiwamo ambapo baadhi ya wanasiasa
watapotea kabisa katika ulingo wa siasa.
Pamoja na mambo
mengine, alisema mwaka huu huenda ukawa mbaya kwa viongozi baada ya utabiri
kuonyesha kuwa viongozi wa dini, kisiasa na wasanii maarufu kuendelea kukumbwa
na kashfa za ngono na ulevi zitakazosababisha anguko lao.
Kwa mujibu wa utabiri
huo, viongozi wa tasnia ya sheria kwa maana ya wanasheria mawakili na majaji
watakumbwa na kashfa hiyo.
“Natabiri kuwapo kwa
vifo vya kawaida na ghafla vya wasanii maarufu duniani ikiwamo Tanzania
vitakavyotokana na fumanizi kuuliwa au kuuana wenyewe, pia kashfa hizo
zitawahusu viongozi wakubwa wa dini, siasa na wasanii maarufu.
“Pia kutawapo kwa
majanga ya moto na mafuriko hapa nchini na duniani kote itakayosababisha
madhara makubwa ikiwamo vifo na madhara mengine na pia kutakuwa ongezeko la
kuibuliwa kwa vitendo vya ufisadi na rushwa,” Alisema.
Alisema mwaka huu
unawataliwa na nyota ya Simba unaashiria vifo vya viongozi wakubwa na maarufu
wa kidini na kisiasa vitakavyotokea kutokana na msongo wa mawazo au shinikizo
la damu.
“Natabiri kuzama kwa
meli kwenye moja ya bahari kuu za dunia na ndege moja ya taifa kubwa duniani
kuanguka na kusababisha vifo vya watu kadhaa,” alisema Maalimu Hassan.
Alisema ili kuepuka
majanga hayo yasitokee watu waache chuki, ubinafsi, choyo, kuchongeana na ngono
isiyokubalika kisheria hasa kwa watawala.
0 Michango:
Post a Comment