![]() |
Mwana wa Rais Yoweri Museveni, Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba na mkewe Charlotte Kutesa Kainerugaba alipokuwa anapandishwa cheo kuwa meja jenerali Mei 25, 2016. |
Mke wa Museveni, Bi Janet
Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alikabidhiwa Juni
mwaka jana.
Jenerali Kainerugaba amekuwa
kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza
operesheni maalum za kijeshi.
Kikosi hicho husimamia ulinzi
wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.
Luteni kanali Don Nabaasa
amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.
Rais Museveni pia amemteua
mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na
kuwa jenerali.
Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali
Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.
Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa
Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha
afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa
Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo.
Watu 100 walifariki wakati wa
operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado
anazuiliwa
Brigidia Peter Elwelu,
aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi yao kuu Mbarara,
amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa kamanda wa majeshi ya
nchi kavu.
0 Michango:
Post a Comment