//
Ads

Mahakama yampeleka Nabii Tito Mirembe

Related image
Tito Onesmo Machibya (Nabii Tito)

MAHAKAMA ya Wilaya ya Dodoma imemuamuru Mkuu wa Gereza la Isanga kumpeleka hospitali kuu ya magonjwa ya akili Mirembe, Tito Onesmo Machibya (Nabii Tito), ili kuchunguzwa kama ana ugonjwa wa akili.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, James Karayemaha amesema anahitaji majibu hayo Machi 5 , 2018 siku ambayo mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Agizo hili linakuja likiwa agizo la awali kutotekelezwa.

Machibya amefikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kufanya uchochezi wa kidini kwa mafundisho anayoyatoa na amekuwa akiieleza mahakama kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ana matatizo ya akili na kuonesha vithibitisho kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Unknown

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment