//
Ads

Kabobe hana akaunti nchini, anaweka fedha kwenye majaba

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema baada ya kumfanyia uchanguzi Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bilble Fellowship, Zakary Kakobe imebaini kuwa Askofu huyo hana akaunti kwenye benki yoyote nchini.

Hayo yameelezwa leo na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere ambapo amesema kuwa wamebaini pia Kanisa la hilo lilikwepa kodi kiasi cha Tsh 20, 834,843.

Amesema kuwa fedha hizo zilizotokana na muwekezaji wa kampuni ya kukuza mitaji na tayari Askofu Kakobe ameshalipa kodi hiyo mara baada ya kufanyiwa uchunguzi huo.

Katika hatua nyingine TRA imebaini kuwa kanisa hilo limekuwa likitunza pesa kwenye majaba na ndoo kinyume na taratibu na kuwa halitengenezi hesabu za mapato na matumizi ya fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi wa fedha.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Unknown

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment