Marehemu Mpoki Bukuku |
Na Mwandishi wetu
Mpiga picha maarufu
Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili katika Taasisi ya Mifupa (MOI) jijini Dar es Salaam, alikokuwa
amelazwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake
zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI)
Almas Jumaa.
"Ni kweli Mpoki
amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya
gari maeneo la Mwenge ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," amesema
Almas.
Mpoki Bukuku amewahi
kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha
magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi
magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.
ð›²
ð›²
0 Michango:
Post a Comment