CHAMA Cha Mapinduzi
(CCM), kimezidi kuogopa kivuli cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
baada ya kutimua wagombea wa uenyekiti wa wilaya ambazo Chadema kimeshinda
ubunge.
CCM kimefuta majina ya wanachama waliopitishwa
kugombea uenyekiti katika wilaya za Hai, Moshi mjini na Siha ambako Chadema
kilishinda ubunge mwaka 2015.
Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Hamprey Polepole ametangaza hayo leo, baada ya kumalizika kikao
cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Polepole amesema
wagombea wote waliofutwa wamebainika kuwa walikuwa na viashiria vya kuhatarisha
uhai wa chama pamoja na kasoro mbalimbali.
Aidha, katika wilaya
ya Musoma vijijini uchaguzi wa ngazi ya mwenyekiti wa wilaya pamoja na jumuiya
zingine utafanyika baada ya chama kutangaza.
Hatua hiyo imefikiwa
baada ya CCM kuamua kupanua wigo na kugawa wilaya za Musoma mjini na Musoma
vijijini.
Amesema kila
mwanachama wa CCM anatakiwa muda wote kuzingatia maadili, kanuni na taratibu
zote za chama na kwamba atakayekwenda kinyume chake atafukuzwa uanachama.
CCM kimetangaza
kwamba hakuna mwanachama atakayeshikilia nafasi mbili kwa wakati mmoja na
kwamba hilo halina mjadala lazima mtu mmoja awe na kofia moja.
Polepole
akizungumzia upande wa Zanzibar, amesema wamepata taarifa kuna watu wameanza
kampeni kwa ajili ya kupata urais visiwani humo kabla ya wakati wake kufika na
kwamba chama kimewaonya.
Kimewataka kuacha
mara moja mpango huo vinginevyo wakibainika kwa ushahidi watatimuliwa ndani ya
chama.
Kwa upande wa
wanachama ambao hawakuridhika na maamuzi ya vikao kwa ngazi waliogombea
wametakiwa kufkata rufaa ngazi ya juu yake ili kuhakikisha haki inapatikana.
Amesema kila mtu
atapata haki yake kwa kufuata tataribu zilizowekwa na chama kupitia vikao.
Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kikao hicho kimepitisha majina ya wenyeviti
161 wa wilaya za Tanzania Bara.
0 Michango:
Post a Comment