//
Ads

Mahakama ya rufaa yakataa kurejesha marufuku ya Trump

Rais wa Marekani, Donald Trump
Na mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Rufaa nchini Marekani imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump ya wasafiri kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.

Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.

Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya juu.

Na muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald Trum aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake ataibuka mshindi.

''Ni uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Na natarajia kufanya hivyo, Tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na ni hali mbaya sana..'' Alisema Trump.

Haki miliki ya pichaTWITTER

Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu. Akizungumza wakati wav kuapishwa kwa Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Rais wa Marekani amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo kuamzia sasa.

Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.

BBC


Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment