//
Ads

Shahidi wa Serikali apataka kigugumizi kumtaja Dikteta


Wakili Peter Kibatala (kushoto) akijadiliana na mteja wake, Tundu Lissu walipokuwa mahakamani 
Na Mwandishi Wetu
SHAHIDI wa pili wa kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amepata kigugumizi cha kumtaja dikteta uchwara katika ushahidi wake.

Shahidi huyo, ASP Kimweli Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi alishindwa kutamka neno dikteta katika kesi hiyo, ambapo Lissu anatuhumiwa kufanya uchochezi kwa kutamka maneno ya kichozi pamoja na kutamka neno “Dikitekta uchwara.”

ASP Kimweli alitoa ushahidi huo leo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Godfrey Mwambapa ambapo alieeleza kuwa terehe 28 Juni mwaka huu katika viwanja vya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu alimsikia Lissu akitoa maneno ya uchochezi;

“… hatuwezi kuvumilia utawala mbovu wa kidikteta uchwara hata kama amechaguliwa kuwa Rais ni lazima apingwe kila mahali.”

ASP Kimweli akiongozwa na Wakili wa Serikali, Mohamedi Salum ambapo alidai kuwa alimshudia Lissu akitoa maneno ambayo yangeweza kuwashawishi wananchi waipinge serikali yao.

Baada ya ASP Kimweli kueleza hayo, Wakili wa Upande wa Utetezi, Peter Kibatala alimuuliza shahidi huyo kuwa dikteta uchwara ni nani mpaka yeye akabaini kuwa ni uvunjifu wa sheria.

Kibatala: Ni sahihi kuwa unayoyaongea mahakamani niliwasikia mnajadili na Wakili Salum hapo nje.
ASP Kimweli: Sio sahihi.
Kibatala: Niliwasikia mkijadili wewe Salumu kuhusu hii kesi hapo nje.
ASP Kimweli: Tumeongea mengi pamoja na masuala kesi
Kibatala: Mpaka unakwenda kituo kikubwa cha polisi cha kati unajua kuwa hilo ni kosa, Je, ni nani aliyetajwa kuwa ni dikteta uchwara.
ASP Kimweli: Simjui, lakini Lissu alisema kuwa hata kama amechaguliwa na wananchi.
Kibatala: Ni sahihi kuwa wapo wengi wanaochaguliwa na wananchi,
ASP Kimweli: Ndio
Kibatala: Je unajua kuwa hapa Tanzania askari wetu wanaenda kupambana vita nchi jirani kupinga utawala wa uonevu na udikteta.
ASP Kimweli: Ni kweli.
Kibatala: Ni sahihi kuwa Mwalimu Nyerere alipinga Udikteta
ASP Kimweli: Ndio
Kibatala: Katika maneno aliyoyasema Lissu alieleza ni nchi gani na apingwe kinamna gani.
ASP Kimweli: Kimya
Wakili mwingine wa upande wa Utetezi, Jeremia Mutasebya aliongeza maswali ambayo yalikuwa magumu kujibiwa kwa upande wa shahidi.
Mutasebya: Ni Kosa au sio kosa kwa mbunge wa upinzani kuwaalika wananchi wawapinge wanasiasa wengine kwa njia ya kupiga kura.
ASP Kimweli: Sio kosa.
Mutasebya: Je kwa ufahamu wako Chama cha Demokrasia na Maendeleo kipo kihalali.
ASP Kimweli: Ndio.
Mutasebya: Ni kosa au sio kosa kwa chama cha upinzani na kukiondoa kukipinga chama tawala madarakani.
ASP Kimweli: Sio kosa.
Mutasebya: Je ni sahihi kwa mbunge wa upinzani kupinga kwa nguvu zote serikali iliyokuwepo madarakani kwa kutumia nia ya kidemokrasia.
ASP Kimweli: Kimya.
Mutasebya: Kwa ufahamu wako Tanzania ni nchi ya kidemokrasia au ya kidikteta?
ASP Kimweli: Demokrasia.
Mutasebya: Je dikteta ni neno la kisiasa.
ASP Kimweli: Ndio..
Mutasebya: Je siku ile kulikuwepo na waandishi wa habari na walitoa zile habari kwenye televisheni, radio na magazeti
ASP: Ndio.
Mutasebya: Katika maelezo yako ulisema kuwa maneno yale yangeweza kusababisha wananchi kushawishika kuipinga serikali yao, Je tangu siku hiyo ulisikia wapi tukio lolote linalotokana na maneno ya Lissu.
ASP Kimweli: Sijasikia.

Kesi hayo imehalishwa mpaka tarehe 18 Januari kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment