//
Ads

Matokeo ya darasa la 7 2017 haya hapa

BARAZA la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dk. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.
Dk.. Msonde amesema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341, 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.
Katibu Mkuu huyo amesema kwamba ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.
Sambamba na matokeo hayo pia Dk. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters – Kagera, St, Severine – Kagera, Alliance ya Mwanza, Sir. John – Tanga, Palikas – Shinyanga, Mwanga – Kagera
Hazina – Dar es salaam, St. Anne Marie – Dar es Salaam, Rweikiza – Kagera na Martin Luther – Dodoma.
Dk. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni Nyahaa – Singida, Bosha – Tanga, Ntalasha – Tabora, Kishangazi – Tanga, Mntamba – Singida, Ikolo – Singida, Kamwala – Songwe, Kibutuka – Lindi, Mkulumanzi – Tanga, Kitwai A – Manyara.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment