//
Ads

Takukuru yakunjua makucha kwa makada wa Chadema

Amani Golugwa
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, amehojiwa na Taasisi ya Kuzuiya na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu vitendo vya rushwa vilivyodaiwa kufanywa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru , Alexander Mnyeti.
Hivi karibu Mbunge wa Arumeru Mashariki alijitokeza kwenye vyombo vya habari akieleza kwa ushahidi wa video namna Mnyeti alivyokuwa akiwashawishi Madiwani wa Chadema kujiuzuru na kukihama chama hicho kwa kutumia (rushwa).
Nassari hakuishia kwa vyombo vya habari bali pia alipeleka Takukuru ushahidi huo aliodai umemnasa Mnyeti akiwashawishi Madiwani wa Chadema kujiuzuru.
Kuhojiwa kwa mwenykiti huyo ni muendelezo wa uchunguzi wa Takukuru ambapo Madiwani wanaotuhumiwa katika sakata hilo wameishahojiwa.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu mguta

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment