//
Ads

Huu ndio mfumo na muundo mpya wa Urais Uturuki

Ubunge:
Idadi ya wabunge kuongezwa kwanzia 550 hadi 600.
Umri wa kuwania ubunge utakuwa 18 badala ya 25.
Uchaguzi wa wabunge na rais utafanyika wakati mmoja baada ya kipindi cha miaka 5.
Rais:
Chama cha kisiasa cha rais na vyama vingine vitakuwa na uwezo wa kuchagua wapiga kura wasiopungua 100,000 na vyama vyenye asilimia 5 ya wapigaji kura wa uchaguzi mkuu .
Masuala yanayohusu mamlaka ya utendaji yanaweza kutolewa na rais.

Rais anaweza kutangaza hali ya dharura nchini ikiwa nchi itakuwa imekumbwa na matukio ya maandamano ,migogoro na ghasia inayoenea nchini na kutishia usalama wa nchi.

Rais atakuwa na uwezo wa kuteua naibu rais zaidi ya mmoja .
Rais atakuwa na uwezo wa kufanya utekelezaji wa baraza kuu.Kwa mujibu wa katiba ya sasa rais ambaye hana mamlaka ya kufanya utekelezaji kwa baraza kuu ,anaweza kuwa na mamlaka ya kuanzisha uchunguzi dhidi ya wananchama wa bunge la Uturuki kama kutakuwa na madai ya kuhusika na kosa.

Amri ya rais inaweza kuondolewa nyakati za hali ya dharura nchini,maamuzi hayatahusishwa na uamuzi wa baraza kuu .
Rais atawakilisha pendekezo la bajeti kwa  bunge la Uturuki.
Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika Novemba 3 mwa 2019.

Baraza kuu la majaji na waendesha mashtaka(HSYK):
Jina la Baraza la majaji na waendesha mashtaka litabadilishwa na kuwa; ‘Baraza la mahakimu na mawakili’.Kutakuwa na bodi ya wanachama 13 katika vitengo 2 .

Wanachama wanne watachaguliwa na rais,huku wanachama 7 wakichaguliwa na bunge la Uturuki.
Katibu wa wizara ya sheria atakuwa atakuwa mwanachama wa asili wa bodi hiyo.

Mahakama ya katiba:
Idadi ya wanachama wa mahakama itapunguzwa na kuwa 15 kutoka 17.
Mahakama ya Jeshi:
Mbali na kuwa na mahakama za kinidhamu ,mahakama za jeshi hazitakuwepo.



Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment