Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humprey Polepole amesema mchakato wa katiba mpya haukufanikiwa kutokana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani na CCM kuweka maslahi yao mbele.
Polepole ameyasema hayo wakati akichangia mada kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Twaweza wa kuwasilisha ripoti yenye jina la "Matarajio na Matokeo: Vipaumbele, utendaji na siasa nchini".
Amesema katiba mpya inaonekana kuwa ajenda katika kipindi hiki ambacho serikali ya CCM imejibu kwa asilimia kubwa hoja zilizokuwa zikionekana ni za vyama vya upinzani, ambazo zimeshughulikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo suala la rushwa.
"Ni dhambi kubwa abisa vyama vya siasa kuanza kuahika bango la katiba mpya kama ajenda yao na kuwaacha mbali wananchi ambao kimsingi katiba ni yao," amesema Polepole.
Amesema tafsiri ya katiba ni kuwaadhibu viongozi wakiwemo wa kisiasa, lakini inashangaza kuona viongozi hao wa kiasiasa wanashika ango la kutaka katiba mpya hali ya kuwa wanajua ni mwiba kwao ni lazima wananchi wajiulize
0 Michango:
Post a Comment