Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' |
Na mwandishi wetu
MBUNGE wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’amelaani kitendo cha mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA
kuzizuia online TV kuendelea kufanya kazi kama TV za kawaida hadi pale
itakapotolewa muongozo na sheria za kuziendesha.
Katazo hilo itaziathiri
baadhi ya TV za mtandaoni zenye umaarufu ikiwemo Ayo TV ya Millard Ayo.
Akiongea bungeni leo mjini Dodoma, Mbilinyi amedai kuwa uamuzi huo unaliingiza
taifa gizani.
“Tunakuwa North Korea
kwa spidi ya ajabu sana,” amesema.
“Tunaonekana wa ajabu
kwenye international community kwa maamuzi kama haya. Kwasababu wananchi wana
haki ya kupata habari kutoka upande wa pili, mfano jana Askofu Gwajima na mfanyabiashara Manji walipata nafasi ya kujibu kwa
haraka sana tuhuma dhidi yao zilizotangazwa kwenye TV pendwa za serikali lakini
wao wasingeweza kupata nafasi ya live kusingekuwa na online TV wakaweza
kujitetea kwa haraka sana,” ameeleza.
“Wananchi sasa wamekuwa
wakitegemea online TV kupata habari za bunge kwahiyo ni wazi suala la kuzuia kwa
namna yoyote online TV ni mwendelezo wa kuzuia wananchi kupata habari za bunge,
ni mwendelezo wa kuliweka taifa gizani.”
Sugu amependekeza kazi
za online TV ziendelee hadi pale sheria hizo zitakapotungwa kwasababu uwepo
wake hakuvunji sheria yoyote.
0 Michango:
Post a Comment