Na Mwandishi
Wetu
KLABU
ya Simba imepata pigo kwa kuondokewa na shabiki wake, Elius Mweta aliyefariki
dunia akiwa uwanjani akishangilia mpira.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, Mweta ambaye
ni mkazi wa Kawe, Dar es salaam alifariki baada ya kupata Shinikizo la moyo
ghafla wakati akishangilia goli la pili la Simba.
Manara
amechukua nafasi hiyo kuwataka wanachama wa Simba katika matawi yao yote
kupeperusha bendera zao klabu hiyo nusu mlingoti kama ishara ya kuomboleza kifo
cha shabiki mwenzao wa Simba.
Aidha
Uongozi wa Simba umeomba wapenzi wa Simba na mpira wa miguu kwa ujumla
kujitokeza kesho saa kumi katika mazishi yatakayofanyika Kawe.
0 Michango:
Post a Comment