Mexence Melo, Mmliki wa Jamii Forum
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa mtandao wa Jamii Forum, Mexence Melo, amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na kesi tatu ikiwemo kuzuia upelelezi wa jeshi la Polisi.
Kwa nyakati tofauti Melo alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka yanayomkabili kwa Mahakimu watatu tofauti.
Katika kesi namba 456 yenye shtaka moja ambalo amesomewa mbele ya Thomas Simba, Hakimu Mkazi Mkuu katika mahakama hiyo na Mohamed Salim, ambapo alidaiwa kuzuia taarifa za upelelezi wa jeshi la Polisi.
Salim amedai kuwa kati ya tarehe Mosi Aprili, tarehe 13 Desemba mwaka huu, huko mikocheni wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaama akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii Media inayoendesha mtandao wa Jamii Forum alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao huo kwa Jeshi la Polisi.
Kesi nyingine namba 457 inayomkabili Melo imesomwa mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa, na Mohmmed Salim wakili wa serikali amedai kuwa mtuhumiwa kati ya tarehe 10 Mei na tarehe 13 Desemba mwaka huu huko Mikocheni, Dar es Salaam akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media inayoendesha mtandao wa Jamii Forum alikwamisha upelelezi wa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za kiupelelezi kwa jeshi la polisi
Melo anakabiliwa na kesi nyingine namba 458 mbele ya Hakimu Victoria Nongwa, ambapo wakili wa Serikali Mohammed Salim alimsomea mashtaka mtuhumiwa ambapo alidai kuwa alikuwa anamiliki mtandao wa bila kuwa na kusajiliwa nchini Tanzania na kuwepewa msimbo wa (dot.tz), ambapo ni kinyume na sheria.
Moja ya mashtaka ya Melo
Salim amedai kuwa kati ya tarehe 9 Desemba, mwaka 2011 na tarehe 13 Desemba, mwaka huu huko Mikocheni akiwa kama Mkurugenzi wa Jamii Media alikuwa anamiliki mtandao wa Jamii Forum bila kusajiliwa nchini Tanzania.
Kosa la pili katika kesi hiyo Melo anadaiwa kati ya Januari 26 na Desemba 13 mwaka huu huko Mikocheni akiwa Mkurugenzi wa jamii media alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi za Jeshi la Polisi.
Mtuhumiwa alitimiza masharti ya dhamana katika kesi namba 456 na 457 pia katika kesi 458 alishindwa kutimiza masharti ambapo iliyopelekea kurudishwa rumande.
Hivyo kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu. Akizungumzia kukosa kwa dhamana kwa mtuhumiwa huyo Jebra Kamboli wakili wa upande wa utetezi amedai kuwa kilichowafanya wakose dhamana ni matakwa ya wadhamini katika kesi hizo ambapo walihitajika wadhamini wawili kwenye kesi namba 458 ambapo walikosekana na kusababisha kurejeshwa rumande kwa mteja wake.
0 Michango:
Post a Comment