Wakati dunia ikisubiri kuona ni nini kitatokea baada ya Robert Mugabe kukataa kujiuzulu licha ya shinikizo kutoka kwa jeshi na chama tawala cha Zanu-PF party, tunaangazia baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kufahamu kuhusu nchi hiyo na hali yake kwa sasa.
1. Uchumi umeporomoka.
Zimbabwe imekuwa ikitoka katika mzozo mmoja wa kiuchumi na kuingia mwingine kwa kipindi cha muongo uliopita. Viwango vya makadirio ya idadi ya watu wasio na ajira ni tofauti, lakini chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo kinadai kiwango cha watu wasio na ajira kilikuwa asilimia 90% mapema mwaka huu.
Zimbabwe imehangaika na hasara kubwa ya kiuchumi, iliyopanda mwaka 2008 ambapo kiwango rasmi kilikuwa ni milioni sawa na asilimia 231 milioni . Nchi hiyo ililazimika kuacha matumizi ya sarafu yake iliyoporomoka dhidi ya dola ya kimarekani na hivyo kutumia sarafu ya kigeni.
Kutokana na kuendelea kwa uhaba wa ukosefu wa fedha taslimu , serikali ilitoa dola yake inayoitwa bond noti, lakini ilishuka thamani yake haraka.
Watu wenye pesa zilizowekwa kwenye benki kwa njia ya kieletroniki hawawezi kuzipata ama hupewa masharti ya kikomo cha kiwango wnachopaswa kukitoa. Kutokana na hili biashara ya pesa kupitia mtandao wa intaneti imekuwa maaruifu.
2. Mugabe amekuwa mwenye utata kwa muda.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93-aliwakanganya wakosoaji wake kwa kubakia madarakani kwa muda mrefu sana. Wakati mwingine akipuuziliwa mbali kama kibonzo anapokuwa ziarani katika nchi za ng'ambo, aliangaliwa na raia wa kawaida wa Zimbabwe kama shujaa wa mapinduzi aiyepigana dhidi ya utawala wa wazungu walio wachache na bado anapata heshma kama "baba wa taifa ".
Lakini yeye na wafuasi wake wametumia ghasia kuendelea kumuweka madarakani, huku wakitumia taasisi za serikali kumnadi bianfsi pamoja na chama chake.
Chama chake kinasema kuwa kinapigana na ubepari na ukoloni, lakini matatizo ya kiuchumi yamekuwa changamoto kwa taifa na wafuasi wake wameathirika pakubwa.
3. Mke wake amesababisha kuangushwa kwa utawala wake
Vita vya kumtafuta mrithi wa Mugabe ambaye anaonekana dhaifu kutokana na umri wa 93wake viliimarika katika miezi ya hivi karibuni.
Chama tawala kiligawanyika mara mbili , upande mmoja ukimuunga mkono mke wake Bi Grace huku upande mwingine ukimuunga mkono mshirika wake wa muda mrefu, Emmerson Mnangagwa.
4. Kiongozi mpya huenda asilete mabadiliko yoyote.
Ikiwa Bwana Mnangagwa aliyeng'olewa mamlakani atamrithi Mugabe kama rais mambo hayatabadilika.
Alitajwa katika maafa yote makubwa na mashambulio dhidi ya wafuasi wa upinzani yaliyotekelezwa wakati wa azma ya kumuweka madarakani Bwana Mugabe.
Hata hivyo , alidokeza kuwa anaweza kuanzisha mageuzi ya kiuchumi , na hata kushirikiana na upinzani katika kuunda serikali ya mpito.
5. Kilichotokea Zimbabwe yalikuwa mapinduzi au la.?
Jeshi liliingilia kati ghafla , hata hivyo bado hawajamuweka madarakani rais.
Katika taarifa yake kwa Televisheni ,jeshi lilisema kuwa linachukua udhibiti wa nchi kwa muda "kuwalenga wahalifu" wanaomzingira mkuu wa nchi, na si Bwana Mugabe binafsi , na bado linamuita kama "amir jeshi mkuu".
Hata hivyo hadi sasa, amekataa kuachia mamlaka, licha ya kwamba chama tawala cha Zanu-PF kimemfuta kiongozi wake , na sasa bunge litalazimika kumshitaki
Hata hivyo, Jumapili, Bwana Mugabe aliapa kubakia kama rais hadi pale mkutano mkuu wa Zanu-PF, unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba utakapofanyika, kwa hivyo haijawa wazi ni nini kitafuatia.
0 Michango:
Post a Comment