Mwigulu Nchemba, Waziri wa mambo ya ndani |
Na Mwandishi wetu
BADO inashangaza
tunakoekelekea na umuhimu wa vipaumbele katika jamii yetu ya Kitanzania!!
Ni
wiki kadhaa sasa tangu kuwepo na kile ninachoweza kuita sakata la Faru kufa, na
hii imepelekea mamlaka kubwa ya Waziri Mkuu kuingilia kati na kudai ushahidi wa
kifo cha mnyama huyo. Lakini pia hili limekuja sambamba na miili ya watu inayookotwa
ikiwa imefungwa na kutumbukizwa Mto Ruvu.
Ni
wazi kuwa, haya ni matukio yanayohitaji utayari wa jamii hasa mamlaka yaani
serikali. Kwa uelewa wangu na matarajio yangu nilifikiri kuwa mwanadamu ana
umuhimu mkubwa labda kuliko mnyama, kumbe hili ni wazo langu tu na labda mawazo
na vipaumbele vya watu na mamlaka havifanani!!
La
kushangaza ni kile ninachokiona kuwa ni upuuziaji wa mauaji ya watu, ambao
umeonekana wazi hasa pale Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliposema
kwa wepesi kuwa hizo maiti ni za wahamiaji haramu na hakuonyesha umuhimu wa
hatua zozote kujua uhakika wa hilo alilolisema. Hata kama ni kweli hao ni
wahamiaji haramu, kifo ndio stahili yao?!!!
Zaidi
ni pale umuhimu wa kujua hao maiti ni nani hautiliwi maanani tena wakati tuko
kwenye hali ya wasiwasi wa watu kupotelewa na ndugu zao. Hatusikii kiongozi
mkubwa kama Waziri Mkuu akionyesha msisitizo wa kufukua maiti hizo ili
zitambuliwe na ikiwezekana sababu za vifo hivyo na ikiwezekana waliohusika
wajulikane na kuchukuliwa hatua. Zaidi Mkuu huyu anaonekana akijikita kutafuta
uhalisia wa kifo cha Faru(Faru John) huku binadamu wakiachwa kama kitu kisicho
na umuhimu. Inashangaza na kutia shaka juu ya umuhimu wa watu katika awamu
hii.
Hapa
Napata maswali kuwa maisha na usalama wa binadamu kipindi hiki sio kipaumbele
muhimu? kwani mnyama anaweza kuchukua
nafasi hata kuliko binadamu?
0 Michango:
Post a Comment