//
Ads

Bei ya umeme yapanda, wateja walalamikia huduma

Felix Ngamlagosi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA
Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5% kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.

Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu  wa EWURA Felix Ngamlagosi amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

Wakati ongezeko hilo likitangazwa, baadhi ya wateja wamelalamikia huduma za Shirika la Tanesco na kulitaka kupanua miundombinu na huduma.


Pia Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.




Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment