Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni rafiki kipenzi wa Papii Kocha mfalme mtoto wa Babu Seya, Bushoke Rutta, ameelezea furaha yake baada ya kusikia rafiki yake huyo ameachiwa kwa msamaha wa Rais, na kwamba ametimiza ndoto zao.
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Bushoke amesema furaha aliyonayo hailezeki kwa alichokifanya Rais na haoni wa kuchukua nafasi yake, kwani alichokifanya ni kitendo cha huruma na upendo wa hali ya juu, kwa kutimiza tumaini ambalo walikuwa nalo rafiki zake hao vipenzi.
Bushoke ameendelea kusema kwamba hivi karibuni rafiki yake huyo alimsikia akisema ana imani Rais wa sasa atawaonea huruma na kuwaacha huru, hata isingekuwa leo basi ingekuwa siku yoyote lakini waliamini hawatafikwa na umauti wakiwa jela.
Akiendelea kusimulia furaha yake Bushoke amesema aliposikia Rais anatangaza kumsamehe Babu Seya na familia yake, mwili ulimsisimka huku asiamini nachokisikia.

Kuhusu Unknown
Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.
0 Michango:
Post a Comment