//
Ads

Zari alivyotua Dar

Wakati mfanyabiashara maarufu Zarina Hassan maarufu Zari Thebosslady akitua nchini Tanzania jana Ijumaa, taarifa zilizopatikana zimeeleza kuwa mzazi mwenzake mwanamuziki Diamond Platnumz yupo nchini Dubai.
Hata hivyo, mtu wa karibu na mwanadada huyo ameliambia Mwananchi kuwa Zari amewasili nchini akitokea Afrika Kusini kwa ajili ya kuzindua duka jipya la bidhaa za nguo linalojulikana kwa jina la Danube.
"Ninachofahamu amekuja kikazi na atakuwepo hapa, uzinduzi ni leo(Jumamosi). Amekuja kwa ajili ya uzinduzi na si kitu kingine." Kilisema chanzo hicho pasipo kutaka kutaja jina.
Hata hivyo taarifa zilizopatikana kutoka kwa ofisi ya mwanamuziki Diamond Platnumz, staa huyo alikuwa nchini Marekani kwa wiki nzima na hii jana alikuwa Dubai ambapo wikiendi hii anatarajiwa kuwepo visiwani Zanzibar.
Ilielezwa kuwa Jumapili mwanamuziki huyo ndipo atawasili jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo Zari amewasili nchini akiwa peke yake bila mtoto yeyote na hata hivyo ameonekana akiwa ameambatana zaidi na watu wanaohusika na uzinduzi huo, lakini kulikuwepo na watu kadhaa kutoka ofisi ya Diamond, akiwemo mlinzi wa staa huyo anayejulikana kwa jina la Mwarabu.
Zari na Diamond waliingia kwenye mikwaruzano baada ya staa huyo kukiri kwamba amezaa na mwanamitindo wa Kitanzania, Hamisa Mobeto.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu mguta

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment