Selemani Msindi (Afande Sele) |
Na
Mwandishi Wetu
SELEMANI Msindi (Afande Sele) msanii
mkongwe wa muziki wa Hip hop hapa nchini na aliyejikita katika masuala ya siasa
baada ya kugombea ubunge Morogoro mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia tiketi ya ACT
Wazalendo ametangaza kujivua chama hicho.
Uamuzi wa Afande Sele unakuja ikiwa ni wiki moja
tangu Habib Mchange, mmoja kati ya waasisi wa chama hicho atangaze kujivua
uanachama wa chama hicho na kuahidi kubaki kama mtanzania asiye na chama.
Ujumbe alioandika Afande Sele kupitia mtandao wa Facebook...
“Leo natangaza rasmi kujivua uanachama
wa chama cha ACT-Wazalendo na sitakua mfuasi wa chama chochote cha siasa bali
nitabaki kuwa raia wa kawaida ndani ya nchi yetu nikiendelea na majukumu
mengine ya kimaisha mpaka nitakavyoamua vinginevyo,” amesema Afande Sele.
Hivi karibuni Afande Sele aliwahi
kueleza kutoridhishwa na viongozi wa ACT, akidai wamekuwa vigeugeu kiasi cha
kumfanya ashindwe kujua iwapo msimamo wa chama hicho ni kuunga mkono upinzani
au chama tawala (CCM).
0 Michango:
Post a Comment