Ndoa ya mtangazaji wa kipindi Take One kinachorushwa na Clouds TV, Zamaradi Mketema imezua mijadala mtandaoni huku wengi wakihoji iwapo ni kazi mpya ya sanaa ya mwandaaji huyo wa filamu ya Kigodoro.
Hata hivyo taarifa zilizosambaa mtandaoni tangu usiku wa kuamkia leo zinaeleza kwamba mtangazaji huyo ameolewa na ndugu wa karibu wa kiongozi mkubwa katika serikali ya awamu ya tano.
Kabla ya ndoa hiyo iliwahi kuelezwa kuwa staa huyo alipata watoto wawili na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba na taarifa ambazo zilisambaa ni kwamba wawili hao huenda wangeoana, hivyo ndoa hiyo inayodaiwa kufungwa kwa siri imewashtua wengi waliokuwa wakiujua uhusiano huo.
Licha ya taarifa hizo kusambaa, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya harusi yake huku sura ya bwana harusi ikiwa haionekani vizuri na kuandika 'Alhamdulilah'.
0 Michango:
Post a Comment