MKuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akibisha hodi kwenye mlango mmoja katika banda linalodaiwa kutumiwa kwa biashara ya ukahaba, katika eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi |
Mwandishi: Hamisi Mguta
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amesema serikali
inatarajia kuvunja nyumba zilizopo Tandale uwanja wa fisi linalosifika kwa
biashara mbalimbali haramu ikiwemo ya ngono.
Makonda ameyasema hayo akiwa Tandale
kwenye mkutano wa hadhara wa ziara yake ya siku kumi jijini humo kujibu maswali
ya papo kwa papo kutoka kwa wananchi wa jiji hilo uliofanyika Shule ya
msingi Tandale.
Akizungumza kwenye mkutano huo Makonda amesema,
serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja
wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na
kujengwa vitegauchumi. badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.
Akiwa katika
eneo hilo baada ya kukatiza vichochoro kadhaa, alifika eneo la klabu cha pombe
za kienyeji, na kuzungumza na mmoja wa wateja waliokuwa wakinywa hapo..
"Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone", Mzee aliyejitaja kwa jina la Mandela, alimtambia Makonda huku akipiga funda la pombe hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa mkoa.
Baadaye alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo.
Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga Makonda, ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika hodi yake.
" Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote. sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu" Kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo.
0 Michango:
Post a Comment