Serikali yasema ipo tayari kugharamia matibabu zaidi ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Antiphas Lissu popote Duniani, pindi itakapopata maombi kutoka kwa familia pamoja na taarifa kutoka kwa madaktari kuhusu mahitaji ya matibabu zaidi ya mgonjwa#Waziri Ummy Mwalimu.
Aidha, Serikali imeshangazwa na taarifa za upotoshaji na dhana ya kuchangishana kwa ajili ya matibabu ya Mhe. Lissu, akiwa Mtanzania na Mbunge, Serikali inayo wajibu wa kugharamia matibabu yake hadi apone ili aweze kuendelea na kazi ya kuwatumikia watanzania na wana Singida Mashariki#Waziri Ummy Mwalimu.
0 Michango:
Post a Comment