Habari zilizotufikia kutoka katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga zinasema mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mama Tatu amemuua mme wake anayejulikana kwa jina la “Mzaramo” kwa kumchinja kisu shingoni na kumchoma kisu tumboni.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamis Septemba 21,2017 katika eneo la Malenge/Uswahilini kata ya Tinde.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule
|
Inaelezwa kuwa wanandoa hao walikuwa amegombana,ndipo mke akamsubiri mmewe alale na alipolala akamchoma kisu tumboni na shingoni.
“Baada ya kutekeleza tukio hilo,mwanamke huyo alifungua radio kwa sauti ya juu kisha kumfunga mlango kwa kufuli kisha kukimbilia Shinyanga Mjini ambapo kuna Mama yake mzazi,alipofika akamwambia mama kuwa amefanya mauaji,hali iliyomfanya mama atoe taarifa polisi na kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa”,mashuhuda wameiambia Malunde1 blog.
“Wanandoa hawa wamepanga nyumbani kwa Kaboja,mme huwa anaonekana mara moja moja hapa Tinde kwa sababu anafanya kazi katika mgodi huko mkoani Geita”,wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
0 Michango:
Post a Comment