Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru) imethibitisha kumshikiria Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake, Mwesigwa Silentine kwa mahojiano ambayo hakuyaweka wazi.
Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibisha kuwa viongozi hao walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi ambapo amesema kuwa Jamal Malinzi na wengine wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.
Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.
Pia alipoulizwa sasa ni lini viongozi hao watafikishwa mahakamani alisema hawezi kusema kwani inawezekana kama watuhumiwa hao wakitoa ushirikiano kwa Takukuru wa ushahidi wanaweza wasifikishwe mahakamani.
0 Michango:
Post a Comment