Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, ametangaza bei elekezi ya zao la ufuta kwa mwaka 2017, Akizungumza Mara baada ya kutangaza kwa bei ya zao hilo, mkuu wa mkoa wa Lindi amesema bei hiyo imezingatia gharama za uzalishaji, na haitohusisha tozo hivyo mkulima atalipwa sh elf mbili kwa kg1.
Sanjari na hilo, ametoa rai kwa wakulima kuungana na kutumia Amcos zao na amezitaka kamati za ulinzi na usalama za ngazi ya wilaya kusimamia suala hilo kwa Lengo la kuwakamata wanunuzi ambao watanunua zao hilo kwa bei ya chini.
Hapa Mahojiono yake na Waandishi wa Habari.
0 Michango:
Post a Comment