//
Ads

Polisi Morogoro waingia mil 11 kwa siku moja


Askari wa Usalama barabarani mkoani Morogoro akisimamia gari la mizigo lililosheheni abiria 

Na Mwandishi Wetu 
JESHI la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani mkoa wa Morogoro kimefanikiwa kukamata makosa 328 ya barabara na kukusanya zaidi ya Sh. 11milioni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa mkoani Morogoro, Ulrich Matei, makosa hayo yalikamatwa siku moja ya Desemba 8, kufuatia oparesheni maalum iliyopangwa na jeshi hilo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Matei amesema, katika oparesheni hiyo jumla ya Sh. 11, 060,000 zilikusanywa kama faini kufuatia makosa mbalimbali yaliyojitokeza.

Aliyataja makosa hayo kuwa ni pamoja na makosa ya upotevu wa nyaraka ambapo walikusanya Sh 25,000, ukaguzi wa magari walikusanya Sh. 165,000, bunduki Sh, 250,000.

Aidha Kamanda Matei alitoa wito kwa madereva kuhakikisha wanaendesha vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani kwa kutoendesha magari mabovu sambamba na kutotumia kilevi.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment