//
Ads

Lema afunguka sakata la Mdee na Bulaya

Baada ya adhabu kutolewa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa wabunge Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda mjini, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka na kudai kwamba haki imenyongwa kupitia wabunge hao.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Lema amedai ni makosa kusema wabunge Mdee pamoja na Bulaya wamesimamishwa vikao ya bunge 2017 na badala yake amedai ni haki imenyongwa kupitia wabunge lakini akiwa anaamini watashinda.

"Tunaposema Mdee/ Bulaya wamesimamishwa vikao vya Bunge 2017 tunakosea.Tunapaswa kusema haki imenyongwa tena kupitia Mdee/Bulaya. TUTASHINDA" - Mh. Lema
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment