//
Ads

Chanjo isiyo salama yaua Sudan Kusini

Na Mwande Mtetezi
SERIKALI ya Sudan kusini imesema watoto wapatao 15 wamekufa ikiwa ni matokeo ya makosa yaliyofanyika katika jaribio la kuwakinga na surua.
Wafanyakazi wa afya katika jimbo la mashariki Ikweta walirudia tena kutumia sindano zisizo na usafi kuwachanja watoto wote.
Waziri wa Afya wa Sudan kusini Riek Gai Kok amesema timu iliyohusika katika kampeni hiyo ya chanjo haikuwa na vigezo wala kupata mafunzo kwa kazi hiyo.
Hata hivyo, huduma za afya zimekuwa zikifanya kazi kwa shida Sudan kusini toka kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.


Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Unknown

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment