//
Ads

Ashikiliwa na Polisi kwa kukutwa na misokoto 824 ya Bangi

Misokoto ya Bangi
MWANAFUNZI wa mwaka wanne wa Kozi ya Uuguzi Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Nelson Matee ameshikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwauzia bangi wanafunzi wenzake pamoja na kukutwa na misokoto 824 ya bangi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Lazaro Mambosasa amesema mwanafunzi huyo yupo mwaka wanne akisomea kozi ya Uuguzi.
Kamanda Mambosasa alisema mwanafunzi huyo alikamatwa na misokoto 824 yenye uzito wa Kilogramu 2.8 aliyokuwa amehifadhi katika mfuko wa Nailoni kwenye chumba anacholala.
Amesema chumba hicho kipo kitivo cha elimu Block B chumba namba 25 katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Kamanda Mambosasa amesema mtuhumiwa amekuwa akifanya biashara  hiyo gharamu takribani miezi minne tangu akiwa chuoni kwa kuwauzia wanafunzi wenzake.
‘’Kwa mujibu wa maelezo ya awali mtuhumiwa wateja wake wakubwa wa madawa hayo ya kulevya aina ya bhangi ni wanafunzi wenzake hii ni taswira mbaya kwa  kwa wanafunzi kutumia madawa ya kulevya’’amesema.
Kamanda Mambosasa amesema mwanafunzi huyo atafikishwa mahakamani kwa kosa la kupatikana na bhangi ambapo alidai operesheni na misako dhidi ya Madawa ya kulevya unaendelea.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment