Rais wa zamani wa Ghana John Mahama |
RAIS wa zamani wa
Ghana John Mahama amelaani uamuzi wa rais wa Marekakani , Donald Trump kwa
kuiondoa Marekani kwenye makataba wa Paris wa 2015 kuhusu mabadiliko ya tabia
nchi.
Mahama alituma ujumbe wake kwa njia ya Twitter,
akiutaja uamuzi wa rais Trump wa kujiondoa kwenye makataba huo wa mazingira
kama " jambo ambalo ni vigumu kuliamini". ''Ni siku ya huzuni sana
katika ushirikiano wa kimataifa ". Uliandikwa ujumbe huo.
Rais huyo wa zamani wa Ghana alikuwa ni
miongoni mwa viongozi wa dunia waliunga mkono makubaliano hayo ya kihistoria
juu ya mazingira mjini Paris, akiahidi kutekeleza hatua za kupunguza hewa ya
makaa duniani.
AliTwitt kwamba Marekani imejiondoa katika
uongozi wake wa dunia.
Trump amesema kuwa mkataba huo
"uliiadhibu" Marekani na utasababisha kupotea kwa mamilioni ya ajira
nchini Marekani.
Wakati huo huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa Koffi Annan ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Afrika
amesema: ''Mabadiliko ya hali ya hewa ni tisho kubwa la enzi yetu, Makubaliano
ya Paris ni matokeo ya makubaliano mengi ya ushirikiano na utashi wa kutafuta
suluhu ya pamoja ya tatizo la dunia.
Hakuna nchi moja inayoweza kuvuruga
makubaliano. Wakati Marekani inajiondoa inadhoofisha mkataba huo wa kimataifa,
haitauvunja " Alisema Bwana Annan.
''Kilichosalia kwa mkataba wa Paris ni kwa
pande zilizosalia kuendelea kujitolea kuongeza juhudi za kutatua matatizo ya
mabadiliko ya tabia nchi''.Wajumbe wa Baraza la Wazee wa Afrika wanasema .
“Ndani ya Marekani kwenyewe, biashara na
mamlaka za majimbo zinaweza na lazima zikchukue hatua pale serikali ya
shirikisho itakaojiondoa,” waliongeza.
0 Michango:
Post a Comment