//
Ads

Bango la mtaa wa Victor Wanyama laibua mapya

Usikose kumtazama kijana huyu mwenye kipaji cha ajabu..


Mpango wa kuondolewa kwa bango la Mtaa uliopewa jina la mchezaji wa soka nchini Uingereza, Victor Wanyama kimeelezwa kuwa umeratibiwa kwa chuki za kisiasa.

Hayo yameelezwa na Boniface Jacob  Meya wa Manispaa ya Ubungo ambaye jana alimkabidhi la mtaa huo kwa mchezaji huyo.

Amesema, aliyeratibu mpango huo ni Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa madai ya kuwa anahakiki kuwa taratibu za  Kuupa jina  Mtaa wa Wanyama zilifutwa ama hazikufuatwa.

Meya Jacob amesema kitendo hicho kimedhihiirisha chuki kutokana na dalili za uwepo wake katika mchakato wa kuupa mtaa huo jina la Mchezaji Wanyama ambaye yupo Nchini kwa Matembezi.

Amese
ma, mchezaji huyo aliyekubali kushiriki kuangalia ligi ya ndondo Cup inayoendelea jijini humo na alionesha nia ya kuwasaidia vijana wa kitanzania wenye hamasa ya kucheza soka lenye tija.

Meya huyo ameeleza kuwa k
itendo hicho ambacho si cha kiungwana kinaweza kumkatisha tamaa mchezaji huyo ambaye angeweza kuwa rafiki nzuri wa Tanzania na kupata tija kupitia mlango wa soka.

hata hivyo amesema taratibu za kuupa jina mtaa huo zilipita kwenye uongozi wa mtaa wa viwandani nao waliriridhia na wana mamlaka kama Serikali ya Mtaa.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment