//
Ads

Mbivu na mbichi uchaguzi Uingereza

Mbivu na mbichi za uchaguzi mkuu nchini Uingereza zitajulikana leo baada ya zaidi ya watu 46.9 milioni wa nchi hiyo kupiga kura.

Upigaji kura utaanza saa 1 asubuhi, (saa za Uingereza) wakati ambapo zaidi ya vituo 40,000 vitafunguliwa kote nchini humo.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wabunge 650 watapigwa kura.

Idadi hiyo ya wapiga kura 46.9 milioni  ni ongezekao kubwa ukilinganisha na  wapiga kura 46.4 waliojiandikisha mwaka 2015.

Kura nyingine tayari zimepigwa  kwa njia ya posta ambazo zilichukua asilimia 16.4 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Vituo vingi vya kupigia kura vimewekwa shuleni na katika vituo vya kutoa huduma za kijamii.

Matokeo ya baadhi ya majimbo yanatarajiwa kutangazwa leo  usiku huku matokeo ya mwisho yakitarajiwa kutangazwa Ijumaa mchana.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment