//
Ads

Aslay awageuka wenzake

Yamoto Band
BAADA ya watu wengi kujiuliza sababu zilizopelekea kundi la Yamoto Band kusambaratika, licha ya kazi nzuri walizokuwa wakifanya, msanii wa bongo fleva katika hilo, Beka Flavour amesema `dogo Aslay' ndio chanzo.

Aslay ambaye alikuwa katika kundi hilo lililomilikiwa na Saidi fella maarufu `Mkubwa fella' ivi karibuni ametoa nyimbo tatu zilizokuwa na ujumbe tofauti bila kumshirikisha mtu hata wenzake waliokuwa kwenye kundi moja.

Beka amefunguka bada ya kuhojiwa katika stori tatu ya Planet bongo ya East Afrika radio ilifanyika jana kwamba mgogoro ulianza baada ya Aslay kutoa wimbo wa kidawa.

Beka ambaye kwasasa anatamba na wimbo `Jibebe' ambao ametoa baada ya kusambaratika katika kundi hilo.
Aliendelea kusema Aslay alitoa wimbo wa `Kidawa' bila hata kumshirikisha mtu yoyote hata viongozi ndani ya Yamoto.


"Baada ya Aslay kutoa wimbo wa `Kidawa' kila mmoja alijiona labda hana uwezo wa kuimba ila tulivyoona hivyo tuliomba kwa uongozi wa Yamoto band ili uturuhusu na sisi tutoe wimbo wa kujitegemea," amesema.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment