//
Ads

Upinzani Tanzania wapata pigo

Philemon Ndesamburo
Na Mwandishi wetu
CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimepata pigo kubwa baada ya kuondokewa na mmoja wa waasisi wake Philemon Ndesamburo.
Akithibitisha taarifa hizo, msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene, amesema Ndesamburo aliyezaliwa mwaka 1935 amefariki leo, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Moshi kwa kipindi kirefu, kupitia CHADEMA, ndiye mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, mpaka hii leo mauti yalipomkuta.
Atakumbukwa zaidi kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa chama hicho cha upinzani, hususan katika kukifadhili chama kwa hali na mali.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu mguta

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment