Taharuki ya Qatar na majirani zake, inaendelea kuongezeka, licha ya wito wa mazungumzo kutolewa.
Safari za ndege zinazotoka Qatar kuelekea Saudi Arabia, Misri na Bahrain zimefutiliwa mbali kuanzia siku ya Jumanne.
Mataifa kadhaa tayari yamekomesha uhusiano wao na kidiplomasia na taifa hiolo lililoko katika rasi ya Arabia, huku yakililaumu kwa "kuunga mkono ugaidi". Doha inakatalia mbali shutma hizo.
Mwaandishi wa BBC wa idhaa ya Kiarabu Amir Rawash, anatathmini namna taharuki kati ya Qatar na majirani zake imefikia kiwango cha kutamausha.
Kundi la Muslim Brotherhood
Baraza la ushirikiano wa mataifa ya ghuba, yanasema kuwa Qatar iliunga mkono upinzani wakati wa vuguvugu lililotokea kwa mataifa ya kiarabu.
Doha, ilionekana kama muungaji mkono wa makundi ya kiislamu, ambayo ilitaka kupata umaarufu katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
Kwa mfano, baada ya kuondolewa kwa Rais wa Misri Mohamed Morsi - kinara mkuu wa Muslim Brotherhood - ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka 2013, Qatar iliwapa hifadhi wanachama wa kundi hilo ambalo limepigwa marufuku na utawala wa Misri.
Saudi Arabia na Milki za kiarabu UAE pia zilitaja Muslim Brotherhood kama kundi "la kigaidi".
Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao rasmi wa habari za utawala wa serikali ya Saudia, Qatar ililaumiwa kwa "kuzikubalia makundi kadhaa ya kigaidi na makundi yenye itikadi kali yenye nia ya kuyumbisha amani katika kanda ya mataifa ya kiarabu, kwa pamoja na makundi kama la Muslim Brotherhood, Daesh (Isis) na Al-Qaeda".
Hata hivyo, Wizara ya nchi za nje ya Qatari, ilisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Riyadh, Abu Dhabi na Manama "hazikuridhisha na yanaegemea madai yasio na msimamo kabisa wala ukweli".
TTaaarifa hiyo aidha inasisitiza kuwa, Qatar inafaa "kujitolea " chini ya mkataba wa GCC na "kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na ugaidi na itikadi kali".
Mbinu ya Iran
Mzozo wa sasa ulianzishwa na taarifa iliyokataliwa iliyomnukuu Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, akikosoa "uadui" wa Marekani dhidi ya Iran.
Qatar ilisema kuwa wadukuzi wanatazamiwa kuchapisha maoni hayo katika shirika lake la habari la taifa.
Saudi Arabia, mpinazi mkuu wa taifa hilo la kiislamu, limekuwa likitatizwa kwa muda mrefu na umaarufu wa Iran katika kanda hiyo.
Mzozo nchini Libya
Libya imekuwa katika lindi la mzozo tangua kuangushwa kwa utawala wa Rais wa nchini Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Kiongozi mkuu wa jeshi ya Libya Khalifa Haftar, ambaye alipata uungwaji mkubwa kutoka Misri, Milki za kiarabu UAE na Qatar, aliilaumu Qatar kwa "kuunga mkono ugaidi".
Haftar anaongoza serikali iliyoko mashariki mwa Libya katika mji wa Tobruk. Ilihali Qatar inaunga mkono serikali pinzani iliyoko katika mji mkuu Tripoli.
Mzozo wa vyombo vya Habari
Mara tu taarifa tatanishi ilipotolewa ikimnukuu Emir wa Qatar mnamo Mei 23, vyombo vya Habari huko UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri yalianzisha ukosoaji mkubwa dhidi ya familia inayotawala Qatar.
Mataifa hayo manne yaliamua kwa kauli moja kuzima mtandao wa habari wa Qatar.
Jumanne jioni Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa kushindwa kwa Qatar, itakuwa mwanzo wa kumalizika kwa makundi ya kigaidi duniani.
0 Michango:
Post a Comment