Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametoa agizo la kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Castory Manase Nkuli (pichani) baada ya kudaiwa kunyang’anya ardhi ya vijiji na kumilikisha kampuni.
Afisa huyo anadaiwa kuchukua ardhi ya ukubwa wa ekari 4,000 ya vijiji vya Ruvu na Mchinga na kuimilikisha kwa kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.
Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji Wizara ya Ardhi Bi. Immaculate Senje amesema utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wanakijiji.
"Hatua ya kwanza kabisa ambayo inafanyika ni kuwaelimisha wanakijiji umuhimu wa kijiji chao kupanda hadhi na kuwa mji mdogo, wakishaelimishwa na wakaelewa unaitishwa mkutano na wananchi wakiridhia muhtasari unaandikwa kuomba ridhaa kutangazwa kuwa eneo la mpango," amesema.
0 Michango:
Post a Comment