//
Ads

Lukuvi: Dar es Salaam imejengwa kiholela

IMEELEZWA kwa katika miji iliyojengwa kiholela ni pamoja na jiji la Dar Es Salaam jambo ambalo linailazimisha serikali kuanzisha mchakato wa kuandaa mastar plani ya jiji hilo.
Kutokana na jiji hilo kuwa kati na majiji ambayo yamejengwa vibaya serikali imesema kwa sasa haitoi hati za kuwamilikisha viwanja bali inatoa hati za kuwarasimisha maeneo ili wakati wa kuboresha mji huo waweze kutambuliwa.
Kauli hiyo ilitolewa leo asubuhi bungeni na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ubungo, Said Kubenea (Chadema). Unaweza kumsikiliza hapa...


Image result for hands arrows


Katika swali la nyongeza la kubenea alitaka kujua ni lini serikali itaweza kupima maeneo ya jimbo lake pamoja na kuweka mipata kati ya kata na kata sambamba na kubainisha mipaka katika jimbo la jirani la Kibamba.
Awali katika swali la mbunge wa Kibamba John Mnyika (Chadema) alitaka kujua katika jimbo la Kibamba ni maeneo gani hayajapimwa na yatapimwa lini.
Pia alitaka kujua kuna mpango gani wa kupunguza gharama za upimaji na utoaji wa hati ili kurahisisha huduma pamoja na kuepusha makazo holela.
Lukuvi akijibu swali la nyongeza la Kubenea amesema, upimaji wa viwanja siyo kazi ya wizara bali ni kazi ya halmashauri ikiwa ni pamoja na kupeleka mafaili kwa kamishina wa ardhi ili yaweze kusainiwa.
Aidha amesema kati ya majiji ambayo yamejengwa vibaya tena kiholela ni pamoja na jiji la Dar es salaam na kutoka na hali hiyo serikali kwa sasa inaandaa mpango mji ili kuweza kulipima upya jiji hilo ili liweze kujengwa vizuri tofauti na sasa.
Katika hatua nyingine Lukuvi amesema kwa sasa wakazi wengi waliopo katika jiji la Dar es salaam hawapewi hati kwa maana ya hati bali wanarasimishwa maeneo ili kuwawezesha watu masikini kutambuliwa katika maeneo yao na itakapofikia uboreshaji watambuliwe.

Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment