Jakaya Kikwete |
RAIS Mstaafu wa Tanzania,
Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la wakimbizi
duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni
mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.
Taarifa kwa vyombo vya habari ilimtaja mstaafu huyo
kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa
maswala ya kigeni nchini Canada Lloyd Axworthy.
Baraza hilo linategemewa kuleta mabadiliko ili
kusaidia kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kimataifa kwa wakimbizi unaeleweka,
unafanyika kwa njia ya usawa na haki, ilisema taarifa hiyo.
Baraza hilo pia litashirikisha madiwani 17 wa
mabaraza.
0 Michango:
Post a Comment