James Comey na rais Trump |
RAIS Donald Trump alimtaka aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la FBI James Comey kusitisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea dhidi ya aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn.
''Natumai utawachana na haya'', bwana Trump aliripotiwa akimwambia Bwana Comey baada ya mkutano katika Ikulu ya Whitehouse mnamo mwezi Februari kulingana na bahrua ilioandikwa na James Comey.
Barua hiyo iliandikwa mara moja baada ya mkutano, siku moja baada ya Michael Flynn kujiuzulu kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Ikulu ya Whitehouse imekana ripoti hiyo katika taarifa.
''Rais Trump hajamtaka bwana Comey ama mtu yeyote kusitisha uchunguzi ikiwemo uchunguzi wowote unaohusiana na jenerali Flynn'', ilisema.
Bwana Flynn alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Februari baada ya kumdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi kabla ya Trump kuchukua mamlaka.
Mgogoro huo wa hivi karibuni kuhusu Urusi ulioripotiwa mara ya kwanza na gazeti la The New York Times unajiri wiki moja baada ya bwana Trump kumfuta kazi Comey kuhusu alivyofanya uchunguzi wa utumizi wa barua pepe za kibinfsi uliotekelezwa na bi Hillary Clinton akiwa waziri.
Kufutwa kazi kwa Bwana Comey kulizua hisia kali nchini Marekani, huku wakosoaji wakimshutumu rais kwa kujaribu kusitisha uchunguzi huo wa FBI kuhusu madai kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani mbali na ushirikiano wa maafisa wa Trump na Urusi.
0 Michango:
Post a Comment