//
Ads

Aliyefanya mauaji akionesha kwenye Facebook asakwa

Steve Stephens anayedaiwa kufanya mauaji huku akirusha moja kwa moja 'Live' kwenye mtandao wa Facebook
Cleveland, Ohio-Marekani


POLISI katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanamtafuta Steve Stephens anayedaiwa kufanya mauaji huku akionesha moja kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.
Maofisa katika mji wa Cleveland wamesema kuwa alionekana akionyesha moja kwa moja mauaji hayo wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima.
Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amesema mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni na amemtaka ajisalimishe mwenyewe.
Polisi wanasema hawajapata ushahidi wa madai ya Stephens ya kuwa alishauwa watu kumi na mmoja.
Sambaza kwenye Google Plus

Kuhusu Anonymous

Hii ni Blog yenye jukumu la kukupasha habari za Mtanzania mwenye hali ya chini ambaye hajapata nafasi ya kutoa maoni yake.

0 Michango:

Post a Comment