![]() |
Jengo la Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam |
Na Mwandishi wetu
UTATA umeibuka
baada ya Asma Juma, mkazi wa Mbande Kata ya
Chamazi jijini Dar es Salaam, kuishutumu Hospitali ya
Wilaya ya Temeke kumuibia mtoto mmoja, baada ya kujifungua pacha.
Mwanamke huyo, alisema kabla ya kwenda kupewa rufaa ya
kujifungua katika hospitali hiyo, alipima kipimo cha ‘ultrasound’ na
kuthibitishiwa kuwa ana mapacha.
Asma alisema awali alikuwa akipata huduma za kliniki katika
Zahanati ya Serikali ya Mbande, lakini alikuwa amefanya vipimo vya ‘Ultrasound’
katika Zahanati ya binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na
kuthibitishiwa kuwa ana pacha.
“Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha
uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nasikia kwa
masikio yangu na kumbukumbu zote nimezihifadhi kwenye kichwa changu.
Ninachotaka ni mtoto wangu,” alisema Asma.
Mganga Mkuu wa
Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo alikiri kuwapo kwa tuhuma hizo na
kusema tayari zinafanyiwa kazi na uongozi.
Source:Mwananchi
0 Michango:
Post a Comment