MTEULE mwengine wa
rais wa Marekani, Donald Trump wa uwaziri wa wanamaji akataa wadhfa huo
Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa Marekani Donald Trump,
kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji amejiondoa baada ya kuonekana
kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa maslahi.
Philip
Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake ya usiri na changamoto
alizokumbana nazo katika kujitenganisha na biashara zake.
Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu
atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.
Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.
Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.
0 Michango:
Post a Comment