Na Mwandishi wetu
IMEBAINIKA baadhi ya madereva
wa Pikipiki au maarufu boda boda mkoani Lindi wamekuwa wanawaweka
wanafunzi shule za msingi na sekondary ujauzito wakati wakiwa bado
shuleni mwaka jana.
Hayo yaliyobainishwa na mkuu wa
mkoa wa Lindi Godfrey Zambi wakati alipokuwa akizungumza na wananchi, viongozi
wa ngazi ya wilaya serikali ya kijiji pamoja na kata ya Litingi, wilayani humo,
alisema kwamba moja ya wilaya kuna wanafunzi wa sekondary saba walipatiwa
ujauzito na madereva hao, mwaka jana.
Tatizo linalowakuta wanafunzi
hao kuomba lifti kwenda shuleni hapo ni moja ya chanzo cha kupatiwa ujauzito
wanafunzi wanaosoma mbali na shule zao kutoka nyumbani kwenda shuleni.
Aliongeza kwa kusema kwamba
wazazi toeni nauli kuwapa wanafunzi siyo mnaawaacha wapewe lifti, ni hatari kwa
vijana hao.
Aidha aliwataka viongozi wa
serikali za vijiji hadi wilaya kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote
wanawaweka wanafunzi mimba.
'Hivi karibuni kuna mzee mmoja
alimweka mimba mwanafunzi sasa yuko ndani anatumikia kifungo.
'Mimi nasema nataka hatua kali
za kisheria zichukuliwe dhidi yao siyo kuwaachia wazazi na wati mimba
kudanganyana'' alisema Zambi.
Alisema kwamba kaaeni macho na
umakini hasa hawa wanafunzi wa kike hizi lifti wanazozitaka ni changamoto ni
lazima wazazi mjitoe kuwasaidia wakiwa bado mashuleni.
Aidha aliwashari wazazi kutoa michango ya
shuleni hasa kwenye ujezni wa vyoo ili kusaidia wanafunzi pamoja na walimu
kukaa maeneo yenye usalama kiafya
0 Michango:
Post a Comment