![]() |
Jenerali Ulimwengu |
Na Mwandishi wetu |
Katika Kesi hiyo namba
moja ya 2017 ambapo Ulimwengu atapeleka Maombi hayo Kesho Mahakama Kuu na
kuomba kuwa Mdai kama Mbowe zidi ya Makonda, Kamanda Wa Polisi Kanda maalumu ya
Dar es Salaam na Mkuu wa upepelezi Cammillius Wambura.JENERALI Ulimwengu
Mwanahabari nguli nchini ameomba kujiunga katika kwenye kesi iliyofunguliwa na
Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (Chadema) zidi Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Awali upande wa wajibu
maombi ambao ni Jamhuri waliwasilisha hoja pingamizi ambapo Mwanasheri Mkuu wa
Serikali Gabriel Malata alidai kuwa maombi hayo yameletwa chini ya sheria
isiyotakiwa na kwamba hayana mashiko. Malata alidai maombi hayo yameletwa nje
ya muda kwa kuwa tayari Mbowe alikamatwa, alifanyiwa mahojiano na aliachiwa na
Polisi.
‘Hati ya kiapo cha
mdai (Mbowe) ina mapungufu kwa sababu kwa mujibu wa sheria kiapo kinatakiwa
kielezee facts (maelezo) na sio mawazo ya mtu hivyo sio sahihi tunaomba maombi
haya yatupiliwe mbali kwa gharama ya kesi,’’ alidai Malata.
Pia alidai kuwa kiapo
hicho ndio kinabeba maombi ya mdai hivyo yakiwa na mapungufu hata maombi yake
yanakuwa na mapungufu.
Malata alidai maombi
hayo yanahusiana na kesi za jinai na kwamba Mahakama Kuu haina mamlaka ya kutoa
maamuzi yanayohusiana na jinai hivyo, wadai walipaswa kupeleka kesi hiyo katika
mahakama husika.
Akijibu mapingamizi
hayo, Wakili Kibatala alidai kuwa mwanasheria wa serikali alitakiwa kuonesha ni
kifungu gani cha sheria ambacho kingeiongoza mahakama katika njia sahihi kuhusu
maombi hayo.
Pia alidai kuwa sheria
iliyotumika kufungulia maombi hayo iko sahihi hivyo kungekuwa na mapungufu
upande wa wadaiwa ungeonesha ni sheria ipi.
Hata hivyo, katika
hoja ya kuingizwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika kesi hiyo
liliibuliwa lakini mahakama iliamuru upande wa wadai urekebisha maombi yao kwa
kuwa hawakumuingiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) licha ya kuishitaki
serikali.
“Tutafanya marekebisho
ya maombi yetu na marekebisho mengine madogo madogo kwa namna tutakavyoona
inafaa siku ya jumatatu na tutawapa wajibu maombi Machi 6, mwaka huu na Machi
8, mwaka huu itatajwa kwa ajili ya kusikiliza maombi hayo,” alidai Lissu.
Katika kesi ya msingi,
Mbowe anaomba mahakama iwazuie wadaiwa kutekeleza azma yake ya kumtia mbaroni
pia itoe amri ya kuwazuia kumkamata hadi hapo kesi hiyo ya kikatiba
itakapomalizika na kwamba polisi wasiendelee na mchakato wowote dhidi yake hadi
hapo kesi hiyo itakapomalizika.
Anadai kuwa sheria
inayompa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kutoa amri ya kumkamata na kumweka ndani mtu
iko kinyume cha katiba, kwa madai kuwa ilitungwa katika mazingira ambayo
hapakuwa na vituo vya polisi vya kutosha. Pia anadai kuwa kwa mazingira ya sasa
sheria hiyo imeshapitwa na wakati na anaiomba mahakama itamke kuwa ni kinyume
cha katiba.
Mbowe pia anadai kuwa
hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa anatekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa sheria
hiyo basi hakutimiza matakwa ya kisheria, ambayo ni pamoja na kutoa taarifa kwa
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au ya Hakimu Mkazi.
Kesi hiyo
itaendele Tarehe 3 Mwezi Machi mwaka huu.
0 Michango:
Post a Comment